Baa la njaa lahatarisha maisha Kusini mwa Afrika

0
332

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) la Umoja wa Mataifa (UN) limesema idadi kubwa ya watu Kusini mwa Bara la Afrika wanakabiliwa na baa la njaa .

Katika taarifa yake mkurugenzi wa shirika hilo Kusini mwa Afrika Lola Castro amesema baa la njaa lipo katika kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa na ushahidi ulioko unaonesha kuwa hali itazidi kuwa mbaya zaidi.

Amesema mabadiliko ya tabianchi pia yamekuwa yakichangia kuathiri nchi hizo na kupelekea mafuriko, ukame na changamoto za kiuchumi hususanI katika nchi za Malawi, Msumbiji, Namibia, Zambia, Zimbabwe, Madagascar, Lesotho, na Eswatini.